• Business Starts Here!

Punguzo la bei ya matangazo ya Kupatana Premium


Punguzo la bei ya matangazo ya Kupatana Premium Punguzo la bei ya matangazo ya Kupatana Premium

Kampuni maarufu ya Kupatana inayokutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa mtandaoni, imeamua kuunga mkono juhudi za serikali kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona nchini.

Hili limekuja baada ya serikali kuchukua hatua za kuzuia mikusanyiko ya watu isiyokuwa ya lazima, kufunga shule za awali hadi vyuo vikuu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huu hatari. 

Tanzania imekuwa moja kati ya nchi nyingi duniani zilizopatwa na mlipuko wa ugonjwa wa Corona. Mnamo tarehe 16 Machi mtu wa kwanza alipatikana na virusi vya Corona nchini. Kupatana imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja wake wanaotumia matangazo ya kulipia yaani Kupatana Premium Ads kwenye jukwaa hilo, ili kuwazezesha  kutangaza bidhaa zao kwa wanunuzi kwa bei nafuu zaidi.

Kupitia jukwaa hilo, wafanyabiashara wataweza kufikisha bidhaa zao kwa wateja ambao wengi wao wako majumbani kwa sasa. Kwa kufanya hivyo, misongamano katika maeneo ya masoko kama Kariakoo itaweza kupungua.

Aidha, wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kama vile simu na vifaa vya nyumbani wanashauriwa kutembelea mtandao wa Kupatana kupitia tovuti au application za simu kuweza kutafuta bidhaa mbalimbali za kununua pasipo kutoka kwenda kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu.

Mamia ya bidhaa mbalimbali zinazouzwa huwekwa kwenye mtandao huo kila siku. Mtu yeyote anaweza kuuza bidhaa yake ikiwa mpya au imetumika kwa kuweka picha ya bidhaa anayouza na kuacha mawasiliano, ambapo mnunuzi anaweza kuwasiliana na mwenye bidhaa na kupanga mahali salama pa kufanya makabidhiano.

Hadi kufikia mwezi Machi, watu zaidi ya 435,382 waliripotiwa kuambukizwa ugonjwa wa Corona na wengine 19,620 kufariki dunia.

Kupatana inawaomba wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya katika kipindi hiki ambacho serikali, pamoja na wadau wengine wakiendelea kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu. 

Contact UsSend Email

  • Tanzanite Tower
  • 128 Sam Nujoma Road
  • Mwenge
  • Kinondoni District
  • Dar es Salaam


Share Product