• Business Starts Here!

TZS 18k - Mmeza fupa


Mmeza fupa Mmeza fupa

SKU: 9789987083794
Categories: Award Winner, Featured, Literary criticism, Literature, New releases, Novel, Swahili
Product ID: 9350

Ali Hilal Ali
Riwaya ya Mmeza Fupa ni riwaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017. Katika tangazo la ushindi wa riwaya hii jopo la majaji lilitoa sifa zifuatazo:

Si mno mtu kukutana na riwaya ya Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, na bila ya kuonesha dalili zozote kwamba imelazimishwa. Wahusika wake wote wamebuniwa kwa ustadi, na kupewa kazi muwafaka za kuziwakilisha tanzu na matabaka mbalimbali ya jamii – pamoja na mikinzano na mazingira yao ya kihistoria, ya kisiasa,ya kisaikolojia, ya kitamaduni, ya kimjini au ya kijijini. 

Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni, maswala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale maswala sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi. Riwaya hii inatudhihirishia mandhari mapya ya utanzu huu wa fasihi ya Kiswahili.

Contact UsSend Email

  • 24 Samora Avenue
  • City Center
  • Ilala District
  • Dar es Salaam


Share Product