• Business Starts Here!

TZS 8,000 - Mirathi ya hatari


Mirathi ya hatari Mirathi ya hatari

SKU: 9789976102451
Categories: Language, Literature, Swahili
Product ID: 302

C.G. Mung’ong’o
Gusto, kijana mdogo wa shule, hakurithi mali ya marehemu baba yake tu, bali pia amerithi tunguri zake, madaraka yake ya kiwanga na mlolongo mzima wa visa, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamtoa Gusto katika ulimwengu wa wachawi. Hatimaye, baada ya kupambana na vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha, inambidi Gusto akate shauri kati ya kuyatekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kuyatimiza matakwa ya dhamiri yake binafsi na ya jumuiya yake inayotafuta maendeleo ya kisasa. 

Mvutano unaotokea unakiuka uwezo wake alioupata shuleni, na kutishia kumrarua vipande vipandeŠ Hiki ni kisa cha kutisha na kutaharakisha, kinachotuingiza katika undani wa uganga wa uchawi na mazingaombwe, na hatimaye kutuacha tukijiuliza kama kweli mambo hayo yanayo manufaa yote kwa jamii yetu au ni doa na mirathi ya hatari tu katika utamaduni wetu.

Contact UsSend Email

  • 24 Samora Avenue
  • City Center
  • Ilala District
  • Dar es Salaam


Share Product