• Business Starts Here!

TZS 11k - Alfu Lela U Lela kitabu cha 9


Alfu Lela U Lela kitabu cha 9 Alfu Lela U Lela kitabu cha 9





SKU: 9789987753079
Categories: Classic, Language, Literature, Short stories, Swahili, Translation
Product ID: 707

Arabian Nights
Mfasiri: Hassan Adam

Hiki ni kitabu cha Tatu katika mfululizo wa hadithi maarufu duniani kote za Alfu Lela U Lela (au Siku Elfu Moja na Moja) zenye asili ya Arabuni na Uajemi. Masimulizi haya ya Alfu Lela U Lela yametafsiriwa kutoka matoleo ya Kiingereza na Kijerumani. Lugha hizi za Ulaya ndimo zilimotafsiriwa hadithi hizi kwa mara ya kwanza kutoka lugha za Kiajemi, Kiarabu na Kihindi. Tafsiri ya Kiingereza ilifanywa na Sir Richard Burton ambaye anafahamika huku kwetu kama mmoja wa wasafiri wa kwanza kutoka Ulaya kutembelea na ati “kuvumbua” sehemu zile walizofika. Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ilifanywa mwaka wa 1928 na katika kufanya hivyo sehemu nyingi zilikatwa au ziliachwa makusudi bila kuzitafsiri kwa sababu wamisionari kawakutaka wasomi wa Kiswahili wasome baadhi ya sehemu kwa sababu zao wenyewe. Matoleo haya, kwa kifupi, ndiyo yenye hadithi kamilifu kwa uhakika; yaani mtiririko wa visa na maana halisi ya hadithi kama zilivyotungwa na kutafsiriwa na magwiji wa lugha hizo mbili zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Kiswahili kina bahati ya kumpata mfasiri, Hassan Adam, Mtanzania mwenye ujuzi wa lugha zote tatu zilizohusika katika kutayarisha tafsiri hizi. Bwana Hassan Adam ni mkufunzi wa miaka mingi katika Taasisi ya Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Cologne, Ujerumani.

Contact Us



Send Email

  • 24 Samora Avenue
  • City Center
  • Ilala District
  • Dar es Salaam






Share Product