• Business Starts Here!

Ofa maalum, Nyumba 5,000 za bei nafuu kwa wote


Ofa maalum, Nyumba 5,000 za bei nafuu kwa wote Ofa maalum, Nyumba 5,000 za bei nafuu kwa wote

AWAMU I: NHC NYUMBA YANGU MAISHA YANGU

Nyumba 5,000 za bei rahisi kwa wote. Zinavutia, bora na za bei nafuu. Miradi yote ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa ina huduma zote za msingi kama Zahanati, shule za chekechea na maduka ya manunuzi. Pia kila nyumba inayojitegemea ina eneo la maegesho ya magari.

Ofa maalum: Lipia kwa pesa taslimu au kwa mkopo kutoka benki washirika (mortgage).

Hatua rahisi za kununua nyumba yako leo: 

 1. Chukua fomu ya kununua kutoka kwenye ofisi za shirika zilizopo mikoa yote au tembelea kwenye tovuti ya shirika (Download hapa)
 2. Rudisha fomu iliyojazwa kikamilifu, ikiambatanishwa na uthibitisho wa malipo ya awali ya asilimia kumi (10%) ya thamani ya nyumba unayotarajia kununua (ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT)
 3. Maombi yako yatapitiwa kwa umakini ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika uhakiki wa watu wanaostahili kulingana na vigezo na masharti ya Shirika la Nyumba la Taifa.
 4. Wateja waliokidhi vigezo na masharti, watapatiwa barua za uthibitisho (Letter of Offer), vile vile wateja ambao hawajakidhi vigezo watafahamishwa kwa njia ya barua. 
 5. Mauzo ya nyumba za mradi husika yatafungwa pindi waombaji waliotoa malipo ya awali watakapofikia asilimia mia moja ishirini na tano (125%) ya idadi ya waombaji.
 6. Mteja atapaswa kuthibitisha utaratibu wa malipo ya asilimia tisini (90%) iliyobakia ya thamani ya nyumba ndani ya kipindi cha siku tisini (90) tangu alipopewa barua ya uthibitisho.
 7. Mteja anaweza kulipia nyumba yake kwa pesa taslimu, malipo ya awamu au kupitia mkopo kutoka benki washirika.
 8. Endapo mteja atashindwa kuthibitisha utaratibu wa malipo ya kumalizia manunuzi ndani ya siku tisini, Shirika litampatia fursa mteja mwingine kati ya waombaji walioko kwenye orodha ya maombi ya mradi husika (waiting list).
 9. Iwapo mteja atashindwa kukamilisha malipo ya asilimia tisini (90%) katika kipindi kilichokubaliwa au amelipa asilimia kumi ya awali (10%) akiwa anasubiri (waiting list) na akakosa nyumba, kiasi alichotoa kinaweza kurudishwa au kuhamishiwa kwenye mradi mwingine iwapo mteja atataka kufanya hivyo.
 10. Shirika la Nyumba litafanya utaratibu wa kutafuta hati za nyumba na kisha kuwapatia wanunuzi waliokamilisha malipo yote ya ununuzi.

Contact UsSend Email

 • Kambarage House
 • 06 Ufukoni Street
 • Upanga East
 • Ilala District
 • Dar es Salaam


Share Product