• Business Starts Here!

Vijana House of Vision
  • Head Office

  • 95 Mwinyijuma Road
  • Mwananyamala A
  • Kinondoni District
  • Dar es Salaam

Vijana house of Vision ni shirika lisilo la serikali lililosajiriwa mwaka 2018 linalotoa huduma za kujitolea kwa jamii. Lilianzishwa na kikundi cha vijana wanaharakati wa kijamii na wakufunzi wa kike. Wajumbe wa shirika hili wote wana uzoefu katika uwanja wa maendeleo na elimu ya kijamii. 

Tunatoa huduma za kujitolea kwa jamii bila kutarajia faida za kifedha huku tukiwa na mtazamo wa kuileta jamii pamoja kutoka sehemu za jamii zisizokuwa na matumaini bila kubagua dini, rangi, kabila, jinsia wala umri.

Watu wote waliokuwa dhaifu kiuchumi na makundi yote ya kijamii yaliyopoteza matumaini, vijana, uwezeshaji wa wanawake, na shughuli za msingi za watoto ndiyo masuala muhimu yanayozingatiwa na shirika letu. Malengo yetu ni kutoa elimu kwa jamii nzima na kukuza hali ya kiuchumi hasa kwa vijana.

- x - x - x - x - x - x - x - x - x - x 

Vijana House of Vision is a non governmental organization registered in 2018. We provide voluntary services to the community. The organization was started by youths' activists with ample experience in community education and community development field.

We provide voluntary services to the community without expectation of financial gain, with a vision to uniting the community, without prejudice to religion, race, ethnic origin, gender or age. 

We pay particular attention to all underprivileged groups in the community who have lost hope including the youth, women empowerment and essential child services. Our aim is to provide education to the community and to develop their economic ability especially to the youth.