• Business Starts Here!

St. Gabriel Technical Secondary School


 • Arusha Road
 • Veyula
 • Dodoma Mjini District
 • Dodoma

Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mtakatifu Gabriel inamilikiwa na Shirika la Mapadre Wapassionist. Shule ipo umbali wa kilomita 20 kutoka Dodoma mjini kwenye barabara kuu ya Dodoma - Arusha katika Kijiji cha Veyula kata ya Makutupora.

Shule ilianzishwa kwa madhumuni makuu mawili:
 • Kuwapatia wanafunzi (vijana) elimu bora yenye kutoa maarifa na ujuzi utakaowawezesha kubuni na kuibua vipaji vyao sambamba na kufanya kazi mbalimbali za ufundi stadi kama vile:
  • Umeme wa majumbani (Domestic Electrical Installation)
  • Useremala (Carpentry and Joinery)
  • Ufundi chuma (Welding and Fabrication)
  • Ufundi bomba (Plumbing)
  • Ushonaji (Designing, Sewing and Cloth Technology)
 • Kuwaandaa wanafunzi kwa masomo ya juu katika vyuo vya ufundi.
Shule hii hutoa baadhi ya kozi hizi kwa miezi mitatu: Kozi zinazotolewa kwa miezi itatu ni:
 • Umeme
 • Useremala
 • Ufundi chuma
 • Ushonaji
 • Ufumaji wa Sweta
 • Udereva
 • Computer
Aidha, Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mt. Gabriel ilianzishwa kwa malengo ya kuwafanya wanafunzi (vijana) wajue na waweze:
 • Kuchagua, kutumia na kutunza vifaa vya kifundi
 • Kukadiria idadi ya gharama za vifaa na utumishi (labour charges) katika kazi inayohusika
 • Kuchora na kusoma ramani mbalimbali za ufundi wa kawaida
 • Kujitegemea kwa kujiajiri kwa njia ya ufundi na ujasiriamali

Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mt. Gabriel ndiyo shule pekee mkoani Dodoma inayotarajiwa kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuunganisha masomo ya kawaida ya sekondari na yale ya ufundi, ikitoa nafasi sawa kwa wanafunzi wa bweni na wa kutwa. Shule ina mazingira bora na ya kuvutia kwa ufundishaji na kujifunza.

MOTTO wa shule ni: 

UBUNIFU, UTIMILIFU, VITENDO NA ELIMU BORA KWA MABADILIKO YA MAISHA 
(CREATIVITY, WHOLISTIC, PRACTICAL AND QUALITY EDUCATION FOR A CHANGE OF LIFE)